IQNA

Iran yatuma meli yake ya tatu ya mafuta Lebanon

22:15 - September 20, 2021
Habari ID: 3474318
TEHRAN (IQNA)- meli ya tatu iliyobeba shehena ya mafuta ya Iran imeondoka hapa nchini kuelekea Lebanon ikiwa ni katika mkakati wa kuvunja vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB limeripoti kuwa, kituo cha ufuatiliaji wa safari za meli cha TankerTrackers kimeeleza katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, meli ya tatu iliyobeba shehena ya mafuta ya Iran imeondoa nchini kuelekea Lebanon.

Sehemu moja ya ujumbe huo wa imesema: Shehena hiyo ya mafuta inaweza kupunguza hali mbaya ya kulemaza ya uhaba wa nishati nchini Lebanon.

Meli ya kwanza ya mafuta ya Iran ilisafirisha shehena ya mafuta hayo kupitia Syria na hatimaye mafuta hayo yakasafirishwa kupelekwa Lebanon kwa kutumia malori.

Syria na Iran zimo kwenye orodha ya nchi zilizoekewa vikwazo na Marekani.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, viongozi mbalimbali wa Lebanon wakiwemo wa kisiasa na kidini wamekuwa wakisisitiza kuwa, kutumwa meli za mafuta za Iran nchini humo kumewezesha kuvunjwa mzingiro wa Marekani dhidi ya nchi hiyo.

Tarehe 19 Agosti, Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah alitangaza kuwa meli zilizobeba mafuta za Iran zinaelekea Lebanon na akatoa onyo kali dhidi ya hatua yoyote itakayojaribu kuchukuliwa dhidi ya meli hizo.

2574441

Kishikizo: iran ، lebanon ، meli ، mafuta
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha