IQNA

21:07 - September 23, 2021
News ID: 3474330
TEHRAN (IQNA)- Duru ya 27 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Croatia imeanza Jumatano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Zagreb.

Kwa mujibu wa taarifa mashindano hayo yana washiriki kutoka nchi 18 zikiwemo Bosnia and Herzegovina, Turkey, Iran, Somalia, Serbia, Ufaransa, Norway, Malaysia, Qatar, Jordan, Marekani, Uhispania, Kuwait na Oman.

Washiriki watashindana katika kategoria mbili za kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu na kuhifadhi nusu yake.

Jopo la majaji katika mashindano hayo linajumuisha  wataalamu na wasomi wa Qur’ani kutoka Croatia, Ufaransa, Macedonia Kaskazini, Uturuki na Bosnia Herzegovina.

Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Waislamu Croatia kwa ushirikiano na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Qatar, Jumuiya ya Kiislamu ya Zagreb na Sekretariati ya Mashindano ya Qur’ani Bara Ulaya.

Katika mashindano ya 26 yaliyofanyika mwaka 2019, wawakilishi wa Iran walishika nafasi ya kwanza na ya pili katika qiraa na kuhifadhi Qur’ani kikamilifu kwa  taratibu.

Croatia Int’l Quran Contest Kicks Off in Zagreb

3999404

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: