Yousef Jafarzadeh na Mehdi Mahdavi wanaiwakilisha Iran katika shindano la mwaka huu. Toleo la 30 la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Croatia yanafanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Ulaya Mashariki kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba kwa kushirikisha wasomaji na wahifadhi Qur’ani kutoka nchi mbalimbali.
Jafarzadeh, ambaye anatoka mkoa wa kusini wa Hormozgan, anashindana katika kitengo cha usomaji wa Qur'ani naya Mahdavi, kutoka mkoa wa kaskazini-magharibi wa Ardabil, atawania tuzo ya juu zaidi ya kuhifadhi Qur'ani nzima.
Wote wawili walikuwa miongoni mwa waliofuzu katika matoleo mawili yaliyopita ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran.
Mtaalamu wa Qur'ani wa Iran Qari Ahmad Abolqassemi alipaswa kuwa kwenye jopo la majaji la tukio la kimataifa la Qur'ani nchini Croatia, lakini kutokana na matatizo ya viza asingeweza kusafiri kwenda Zagreb.
Mwaka jana, Ali Gholam Azad wa Iran alishika nafasi ya tatu katika kategoria ya kukariri toleo la 29 la shindano hilo.
3490041