IQNA

Mazungumzo

Mkuu wa ICRO, Waziri wa Utamaduni wa Croatia wsisitiza ukuzaji wa mijadala ya dini mbalimbali

17:59 - November 06, 2024
Habari ID: 3479712
IQNA-Mkuu wa Shirika la Iran Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO) na waziri wa utamaduni wa Croatia wanesisitiza umuhimu wa kuendeleza mazungumzo ya dini mbalimbali kati ya Iran na Croatia.

Mkuu wa ICRO, Hujjatul-Islam Mohammad Mehdi Imanipour na Nina Obuljen Korzinek walikutana Zagreb baada ya duru ya tatu ya mazungumzo ya dini tofauti kati ya Kituo cha ICRO cha Mazungumzo kati ya Imani na Tamaduni na wanafikra wa kidini wa Croatia.

Katika kikao hiocho Waziri wa Utamaduni wa Croatia ametoa wito wa kuitumia tajiriba na uzoefu wa wafuasi wa dini tofauti nchini Iran katika kustawisha utamaduni wa kuishi pamoja kwa amani na masikilizano watu wa dini mbalimbali.

Nina Obuljen Koržinek amesema baadhi ya watu wenye misimamo ya kufurutu mpaka huwa sababu ya kuenea chuki na upinzani dhidi ya shughuli za kidini.

Koržinek ameongeza kuwa, baadhi ya watu wenye ushawishi huchochea tofauti na mifarakano kwa maslahi yao binafsi.

Waziri wa Utamaduni wa Croatia amesisitiza kwamba, katika hali hiyo, mazungumzo kati ya dini mbalimbali yanakuwa na umuhimu maradufu na kufafanua kuwa, mazungumzo na majadiliano yanaweza kutatua sutafahamu na hali ya kutoelewana; na ni kwa sababu hiyo Croatia inataka kuandaliwe mazingira ya kuwepo tamaduni kadhaa na dini mbalimbali ulimwenguni.

Duru ya tatu ya mazungumzo ya kidini kati ya Kituo cha Mazungumzo Baina ya Dini na Tamaduni Mbalimbali cha Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu la Iran na wanafikra wa kidini wa Croatia inafanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Zagreb.

Mada kuu ya duru hii ya mazungumzo ambayo yameandaliwa na Baraza la Dini la Croatia na kusimamiwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Croatia, imetajwa kuwa ni "Tajiriba Zilizopatikana Katika Mazungumzo Baina ya Dini Mbalimbali".

/3490583

 

 

Habari zinazohusiana
captcha