IQNA

Hujuma ya kigaidi katika msikiti mjini Kabul, Afghanistan

13:40 - October 04, 2021
Habari ID: 3474380
TEHRAN (IQNA)- Raia wasiopungua watano wamepoteza maisha baada ya bomu lililotegwa mlangoni mwa msikiti wa Eid Gah mjini Kabul, kuripuka na kuwajeruhi watu wengine kadhaa waliokuwa wanahudhuria ibada ya kumbukumbu ya mama wa msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid.

Rais wasiopungua watano wamepoteza maisha baada ya bomu lililotegwa mlangoni mwa msikiti wa Eid Gah mjini Kabul, kuripuka na kuwajeruhi watu wengine kadhaa waliokuwa wanahudhuria ibada ya kumbukumbu ya mama wa msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid.

Hadi sasa hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulio hilo, lakini Tangu Taliban ilipochukua udhibiti wa Afghanistan katikati ya mwezi Agosti, mashambulizi yanayofanywa na kundi la kigaidi la ISIS dhidi ya Talib yamaneongezeka.

Kuna hofu ya kuenea mgogoro mkubwa zaidi kati ya makundi hayo mawili hasimu huku ISIS inaendelea kudhibiti maeneo ya Mashariki ya Nangarhar.

 Kundi la Taliban linasema hujuma dhidi ya misikiti nchini Afghanistan zinatekelezwa na mashirika ya kijasusi ya maadui.

Taliban inasema hujuma za hivi karibuni dhidi ya misikiti, mazishi, hospitali na uharibiufu wa miundo msingi ni sehemu ya njama za maadui wanaolenga kueneza hofu na wahka ili kuvuruga mchakato wa amani nchini humo.

4002137

Kishikizo: taliban isis msikiti kabul
captcha