IQNA

Waislamu zaidi ya 60 wauawa aktika hujuma ya kigaidi msikitini Afghanistan

19:46 - October 08, 2021
Habari ID: 3474397
TEHRAN (IQNA)- Waumini zaidi ya 60 wameopoteza maisha katika hujuma kigaidi dhidi ya msikiti wa Waislamu wa madhehebu ya Shia huku katika mji wa Kunduz kaskazini mashariki mwa Afghanistan.

Waumini wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo iliyojiri wakati wa Sala la ijumaa na hadi sasa hakuna kundi lololte lililodia kuhusika katika hujuma hiyo. Hujuma kama hizo zimekuwa zikitekelezwa na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Naibu Waziri wa Habari na Utamaduni katika utawala wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema serikali imeanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo. Katika ujumbe wake wa Twitter, Mujahid amesema: “Leo adhuhuri kumejiri mlipuko katika msikiti wa ndugu zetu Mashia ambapo ndugu zetu kadhaa wameuawa shahidi na kujeruhiwa.”

Siku chache zilizopita, raia wasiopungua watano walipoteza maisha baada ya bomu lililotegwa mlangoni mwa msikiti wa Eid Gah mjini Kabul, kuripuka na kuwajeruhi watu wengine kadhaa waliokuwa wanahudhuria ibada ya kumbukumbu ya mama wa msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid.

 Kundi la Taliban linasema hujuma dhidi ya misikiti nchini Afghanistan zinatekelezwa na mashirika ya kijasusi ya maadui.

Taliban inasema hujuma za hivi karibuni dhidi ya misikiti, mazishi, hospitali na uharibiufu wa miundo msingi ni sehemu ya njama za maadui wanaolenga kueneza hofu na wahka ili kuvuruga mchakato wa amani nchini humo.

4003142

captcha