IQNA

Sherehe za Maulidi ya Mtume SAW zafanyika katika misikiti ya Istanbul, Uturuki

15:42 - October 18, 2021
Habari ID: 3474437
TEHRAN (IQNA)- Sherehe za kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad SAW maarufu kama Milad un Nabii au Maulidi zimefanyika Jumapili jioni katika misikitini mbali mbali ya mji mkubwa zaidi Uturuki, Istanbul.

Kwa mujibu wa taarifa, misikiti mikubwa kote Istanbul imeandaa sherehe za Maulidi ambazo zimehudhuriwa na idadi kubwa ya waumini waliojawa furaha.

Sherehe hizo ambazo aghalabu zilifanyika baada ya Sala ya Ishaa zilijumuisha qiraa ya Qur'ani Tukufu, hotuba kuhusu Sira ya Mtume SAW na pia qaswida.

Kati ya misikiti iliyoshuhudiwa sherehe kubwa ni ile ya Sultan Ahmed, Hagia Sophia, Suleimaniye na Fatih.

Uturuki ni nchi ya Kiislamu katika eneo la Asia Magharibi na asilimia 99 ya wakazi wake ni Waislamu.

Kuhusiana na kuzaliwa Bwana Mtume SAW kuna riwaya mbili mashuhuri. Waislamu wengi wa madhehebu ya Kisuni wanaamini kwamba, Bwana Mtume SAW alizaliwa tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal mwaka wa tembo uliosadifiana na mwaka 570 Miladia.

Kundi jengine la Waislamu ambalo linaundwa zaidi na Waislamu wa madhehebu ya Shia Ithanaashari linaamini kwamba, Mtume wa Uislamu alizaliwa tarehe 17 Mfunguo Sita Rabiul Awwal mwaka huo huo. 

Kwa ujumla Waislamu huadhimisha Maulidi katika mwezi mzima wa Rabiul Awwal na katika baadhi ya nchi sherehe hizo huendelea hata katika mwezi unaofuata wa Rabiu Thani.

برگزاری مراسم بزرگداشت ولادت رسول اکرم (ص) در مساجد استانبول + عکس
 
3476095

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha