IQNA

Maulid ya Mtume Muhammad SAW

Mkutano wa Milad-un-Nabi wafanyika Algeria

18:41 - October 11, 2022
Habari ID: 3475913
TEHRAN (IQNA) – Mkutano wa 11 unaoandaliwa kila mwaka kwa mnasaba wa Maulid ya Mtukufu Mtume (SAW) ulifanyika katika mji wa Adrar nchini Algeria.

Shule ya Qur'ani ya Malik ibn Anas huanda hafla hiyo kila mwaka ambapo mwaka huu imehudhuriwa na wasomi, wanafikra, na watu mashuhuri wa vyuo vikuu kutoka sehemu tofauti za nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Mada ya kongamano la mwaka huu ilikuwa "Uhusiano wa Kidini na Kitamaduni wa Algeria na Afrika Magharibi".

Mohammad al-Mahdi Gheytawi, mkufunzi wa Shule ya Qur'ani ya Malik ibn Anas amesema mada hiyo imechaguliwa kwa ajili ya kuwaenzi wale waliochangia katika kukuza uhusiano kati ya Algeria na nchi za Afrika Magharibi.

Washiriki walitoa wito wa kuanzishwa kwa kituo cha televisheni cha kutangaza vipindi kuhusu uhusiano wa Algeria na Afrika Magharibi katika nyanja tofauti za kitamaduni, kijamii na kiuchumi.

Kumefanyika miadhara  katika sehemu tofauti za Algeria katika siku za hivi karibuni za kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu Muhammad (SAW)

 Jumapili, Oktoba 9, ilikuwa ni siku ya 12 ya mwezi wa Hijri wa Rabi al-Awwal, ambayo, kwa mujibu wa Waislamu wa Kisunni, huadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Waislamu wa madhehebu ya Shia duniani kote husherehekea hafla hiyo ya kipekee siku ya 17 ya Rabi al Awwal, ambayo mwaka huu inasadifiana na  Ijumaa, Oktoba 14. Sherehe hizo za kukumbukza kuzaliwa Mtume Muhammad SAW ambazo pia ni maarufu kama Maulidi au Milad-un-Nabi hufanyika kwa muda wa takribani miezi miwili mfululizo.

4091083

captcha