Wasomi hao wamesisitiza upendo wao kwa mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu na pia wamesisitiza umuhimu wa kukuza mafundisho na maadili ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) ili kueneza amani na udugu baina ya watu.
Naba al-Himami Mkuu wa Taasisi ya Utafiti na Mafunzo ya Kiislamu yenye mafungamano na Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ali (AS) huko Njama imesema kuwa mkusanyiko huo ni sehemu ya mipango ya Wiki ya Sadiqayn Duniani iliyofanyika kwa mwaka wa pili kwa mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) na Imamu Sadiq (AS).
Amesema wawakilishi kutoka dini tofauti na madhehebu za Kiislamu kutoka Iraq na nchi nyingine walishiriki katika vikao hivyo.
Al-Himami ameongeza kuwa, kushiriki wanachuoni na wafuasi wa dini tofauti katika hafla hiyo kunaonyesha kuwa mapenzi kwa Mtume Muhammad (SAW) na Ahl-ul-Bayt (AS) yanawaleta pamoja watu wote bila ya kujali tofauti zao.
3489983