IQNA

Hamas yaipongeza Algeria kwa kupinga uhusiano na Israel

16:56 - November 13, 2021
Habari ID: 3474549
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeipongeza Algeria kwa kupinga uanzishwaji uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Msemaji mwandamizi wa Hamas, Sami Abu Zuhri amepongeza msimamo thabiti wa Algeria wa kupinga na kukosoa uanzishwahi uhusiano wowote ule baina ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendelea kuzikoloni na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Abu Zuhri amesema msimamo huo imara wa Algeria unazuia njama za wazayuni kujipenyeza zaidi katika nchi za Kiarabu na Afrika.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra alitoa wito kwa nchi za Kiarabu kuunga mkono taifa la Palestina badala ya kuusaidia utawala wa Kizayuni wa Israel kueneza satwa yake katika nchi ya Kiarabu.

Lamamra aliwalaani baadhi ya maafisa wa Libya ambayo wametoa matamshi ya kuunga mkono uanzishwaji uhusiano wa kawaida na Israel na kuyataja kuwa 'yasiyo ya uwajibikaji' na kuongeza kuwa misimamo kama hiyo haisaidii hata kidogo jitihada za kurejesha amani katika eneo.

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa kuwa jenerali muasi Libya Khalifa Haftari ameahidi  kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Libya katika uchaguzi ujao Disemba mwezi ujao.

Akizungumza katika mahojiano na Televisheni ya Taifa ya Algeria, Ramtane Lamamra amesema kuwa, nchi yake inafadhilisha kuingia madarakani nchini Libya viongozi ambao wanapenda nchi yao, wanatanguliza mbele maslahi ya taifa ni si wenye kuingia katika mahesabu ya ajinabi kwa ajili ya maslahi ya watu wengine.

Ikumbukwe kuwa mwezi Agosti pia, Algeria ilipinga vikali hatua ya mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika kuupa utawala haramu wa Israel hadhi ya mwanachama mwangalizi katika umoja huo. Algeria imeonya kuwa, hatua hiyo hatimaye itapelekea kuvunjika Umoja wa Afrika.

Tokea ipate uhuru wake, Algeria imekuwa mstari wa mbele katika kutetea ukombozi wa taifa la Palestina.

 4012693

Kishikizo: algeria ، hamas ، palestina ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha