IQNA

Kundi la ISIS (DAESH) lasema limehusika na mashambulizi ya kigaidi Uganda

12:16 - November 18, 2021
Habari ID: 3474575
TEHRAN (IQNA)- Kundi la kigaidi la ISIS limetoa taarifa na kudai kuwa limehusika na hujuma za kigaidi nchni Uganda Jumanne.

Watu wanne walipoteza maisha kufuatia mabomu mawili yaliyoripuka Jumanne Novemba 16, 2021 katika mji mkuu wa Uganda, Kampala na kupelekea kufungwa bunge la nchi hiyo.

CNN imenukulu kituo cha habari cha Amaq kinachofungamana na ISIS kikidai kuwa wapiganaji watatu wa kundi hilo ndio waliotekeleza hujuma hiyo ya kigaidi.

Awali maafisa wa polisi Uganda walisema hujuma hiyo ilitekelezwa na kundi la waasi wa ADF walioko kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Imedokezwa kuwa washambuliaji wawili waliokuwa wakiendesha pikipiki za abiria maarufu kama boda boda walijilipua karibu na lango la jengo la bunge  huku mshambuliaji wa tatu alilenga kituo cha upekeuzi cha polisi. Mashambulizi hao kati kati mwa jiji la Kampala yaliachana kwa dakika mbili punde tu baad aya saa nne asubuhi. Polisi wanasema walizuia shambulizi la tatu baad aya kupata bomu katika nyumba ya gaidi aliyekuwa akilenga kutekeleza mashambulizi.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewataka maafisa wa polisi kuchukua tahadhari na kuimarisha doria katika vituo vya basi, migahawa, makanisa, misikitni na katika masoko.

3476533/

captcha