IQNA

Waislamu wa Kosovo wapata chanjo ya COVID-19 baada ya Sala ya Ijumaa

13:51 - November 20, 2021
Habari ID: 3474582
TEHRAN (IQNA) Wakuu wa afya nchini Kosovo wanashirikiana na viongozi wa Kiislamu katika kuwashawishi watu wengi zaidi wapate chanjo ya COVID-19.

Katika kufikia lengo hilo kumefanyika zoezi la kudunga chanjo ya COVID-19 baada ya Sala ya Ijumaa katika misikiti kote Kosovo. Maimamu nchini humo wamewahimiza waimuni kudungwa chanjo hiyo punde baada ya Sala ya Ijumaa jana.

Pamoja na kuwa maambukizi ya COVID-19 yamepungua Kosovo, lakini wakuu wa nchi hiyo wana wasiwasi kuwa yamkini wimbi jipya la maambukizi likaibuka msimu wa baridi na hivyo wanasisitiza kuwa chanjo ndio njia bora zaidi ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Kumeshuhudiwa ongezeko la watu ambao wanaochanjwa kutoka 20,000 kwa siku mwanzo wa mwezi Machi hadi chini ya 2,000 kwa siku hivi sasa. Hadi kufikia sasa ni asilimia 42 ya watu wote milioni 1.8 wa Kosovo ndio waliopata chanjo ya COVID-19.

"Huu ni ubunifu mzuri sana. Naishukuru jamii ya Kiislamu, serikali na wizara ya afya kwa ubunifu huu ambao kwa kweli unahitajika," amesema Rzhdi Zhita, mfanyakazi aliyestaafu ambaye alipata chanjo yake baada ya Sala ya Ijumaa.

Imam Burhan Hashani wa Msikiti wa Sultan Muhammad II mjini Pristina ni miongoni mwa wanaohimiza Waislamu wapate chanjo.

"Ni mara ya kwanza namsikia Imamu akitaka watu wachanjwe. Natoa wito kwa wote wachanjwe," amesema Egzon Daka, kijana aliyeswali katika msikiti huo.

/3476558

Kishikizo: kosovo ، covid 19
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha