IQNA

Watoto na Qur'ani

Watoto 1,000, vijana wanajifunza Qur’ani katika Chuo cha Kukariri cha Kosovo katika Miaka 7

21:59 - September 09, 2024
Habari ID: 3479405
IQNA - The "Little Memorizers" Academy ni taasisi huko Pristina, mji mkuu wa Kosovo, ambayo inafundisha Qur'ani kwa watoto.

Watoto 1,000, vijana wanajifunza Qur’ani katika Chuo cha Kukariri cha Kosovo katika Miaka 7

IQNA - The "Little Memorizers" Academy ni taasisi huko Pristina, mji mkuu wa Kosovo, ambayo inafundisha Qur'ani kwa watoto.

Taasisi hiyo ilizinduliwa na dada wawili wa Kosovo ambao ni wahifadhi wa Qur’ani Tukufu.

Katika kipindi cha miaka saba, tangu waanzishe  chuo hicho, wameweza kufundisha kuhifadhi na kusoma Qur'ani kwa zaidi ya watoto na vijana 1,000.

Mbali na watoto wa Kosovo, mamia ya watoto wa Albania wanaoishi katika nchi tofauti kama vile Italia, Austria na Uswizi wamesoma kozi za mtandaoni za majira ya joto zilizoandaliwa na taasisi hiyo.

Dada hao wawili, Renita na Fatima Nitaj, wanasema kwamba mapenzi kwa Quran yalipandikizwa katika mioyo yao na wazazi wao.

Walianza safari yao na Quran wakiwa na umri wa miaka 7, wakihudhuria madarasa ya Qur’ani wakati wa likizo za kiangazi na wakati wa mwaka wa shule.

Wamefaulu katika nyanja ya Qur'ani na shuleni na chuo kikuu.

Wana shaza za kwana na uzamili  katika Masomo ya Kiislamu kutoka Kitivo cha Mafunzo ya Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Pristina.

Baada ya kuhifadhi Qur’ani kikamilifu kwa moyo, wawili hao waliamua kutimiza matakwa yao ya pili: kuwafundisha watoto Qur’ani. Ndio maana walianzisha chuo hicho cha tahfidh au kuhifadhi Qur’ani, ambapo watoto hujifunza kuhifadhi na kusoma Qur’ani.

3489807

Walianza chuo hicho wakiwa na wanafunzi watatu tu na hadi sasa watoto na vijana 1,000 wamejifunza Qur’ani  katika taasisi hiyo.

Kishikizo: qurani tukufu kosovo
captcha