IQNA

Harakati za Qur'ani

Wanafunzi wa Kike wa Qur'ani waenziwa Kosovo

20:03 - October 30, 2024
Habari ID: 3479672
IQNA - Sherehe ilifanyika mashariki mwa Kosovo kuwaenzi wasichana 44 ambao wamehitimu kutoka kozi za Qur'ani.

Wasichana hao walio katika rika tofauti wamemaliza masomo ya kusoma Qur'ani yaliyofanyika katika Msikiti wa Dar al-Mahal.
Hafla hiyo maalum iliandaliwa na maafisa wa msikiti na walimu kwa uratibu na idara ya wanawake ya ofisi ya rais wa Kosovo.
Ilikuwa ni sehemu ya juhudi za kuunga mkono ukuzaji wa mwamko wa kidini miongoni mwa wanawake na wasichana nchini humo.
Misikiti ya Kosovo ina walimu 150, wengi wao wakiwa wamehitimu vyuo vikuu katika fani za mafundisho ya Kiislamu.
Kosovo ni nchi yenye imani nyingi, na makabila tofauti katika eneo la Balkan la Ulaya ya Kusini-Mashariki. Ingawa nchi hii  haina dini rasmi, karibu asilimi 96 ya wakazi wake ni Waislamu.
Nchi hiyo huwa na mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kila mwaka na washiriki kutoka nchi kama Uturuki, Macedonia, Bosnia na Herzegovina na Albania.
Mashindano hayo hulenga kueneza utamaduni wa Qur'ani na kuendeleza usomaji wa Qur'ani miongoni mwa Waislamu.

3490477

Habari zinazohusiana
captcha