IQNA

17:24 - January 25, 2022
Habari ID: 3474853
TEHRAN (IQNA)- Wakuu wa Saudi Arabia wametoa amri kuwa wafanyakazi katika misikiti waajiriwe kikamilifu na wasiwe wanafanya kazi maeneo mengine.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu Saudia Abdulatif Al Sheikh ametoa dikriii kuwa,  wafanyakazi wote wa misikiti hawapaswi kuwa na kazi zingine. Waziri hiyo ametoa maelekezo ya kufuatwa na wafanyakazi wanaohudumi misikitini ambapo misikiti itatayarisha orodha ya wafanyakazi wake.

Kwa mujibu wa kanuni hiyo mpya wale walio na kazi ya pili nje ya msikiti hawataruhusiwa kuendelea kuhudumu misikitini.

Hakujatolea maelezo mengine rasmi kuhusu dikrii hiyo wala hakuna taarifa kuhusu idadi kamili ya wafanyakazi wanaohudumu misikitini Saudia.

3477533

Kishikizo: saudia ، msikiti
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: