IQNA

Waziri wa Teknolojia Pakistan

Soko la sekta ya ‘Halal’ dunaini linastawi kwa kasi

22:48 - December 25, 2021
Habari ID: 3474721
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Sayansi na Teknolojia Pakistan amesema soko la sekta halali duniani linastawi kwa kasi na yamkini pato lake likafika matrilioni ya dola katika mustakabli wa karibu.

Shibli Faraz amesema serikali imeidhinisha kauni za kibiashara za Mamlaka ya  Halal ya Pakistan na Idara ya Vyeti vya Halal Pakistan.

“Ni hatua kubwa iliyoweza kufikiwa na Mamlaka ya Halal Pakistan,” amesema  Faraza katika kikao cha wadai kuhusu kufahamu kanuni za sekta ya Halal na namna bidhaa Halal za Pakistan zinavyoweza kuuzwa katika soko la kimataifa. Aidha amesema kuna uwezekano wa sekta ya Halal kuwa na thamani ya matrilioni ya dola.  Hivi sasa nchi zinazoongoza katika uuzaji wa bidhaa Halal duniani ni nchi zisizo za Kiislamu kama vile Brazil, Australia, Thailand, China, Korea Kusini na Afrika Kusini.

Uchumi 'Halal' umejengeka katika msingi wa mahitajio ya Waislamu zaidi ya bilioni 1.6 duniani ambao wanataka bidhaa na huduma ambazo zinaenda sambamba na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Ili kuzalisha bidhaa au kutoa huduma halali si lazima mwenye kufanya hivyo awe Mwislamu.

Uchumi 'Halal' duniani unakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya   dola trilioni  3 na umetajwa kuwa sekta inayokuwa kwa kasi zaidi duniani.

3477079

Kishikizo: halal uislamu pakistan
captcha