IQNA

23:24 - May 10, 2022
Habari ID: 3475233
TEHRAN (IQNA)- Maonyesho ya kipekee kwa ajili ya wanaotaka mtindo wa kimaisha ambao ni ‘Halal’ katika eneo la Amerika Kaskazini yanafanyika wiki hii nchini Canada kwa lengo la kuwaunganisha watenda na mashirika yanayojishughuisha na bidhaa na huduma Halal.

Kutakuwa na maonyesho pamoja na kongamano  la ‘Halal Expo Canada’ kuanzia Mei 12-14 katika Kituo cha Kimataifa cha Toronto.

“Kama lango la kuingia soko la Halal la Amerika Kaskazini, maonyesho ya ‘Halal Expo Canada 2020’ yataleta pamoja bidhaa na huduma za hali ya juu zaidi katika sekta ya halal,” imesema taarifa katika tovuti ya maonyesho hayo.

“Kutoka chakula na vinywaji hadi dawa na vipodozi, huduma za kifedha na utalii, sekta yote Halal itajumuika katika paa moja ambalo watakuwemo wafanyabaishara na wateja.”

Sekta ya Halal Canada inakadiriwa kuwa yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 1.2 na inaendelea kustawi kutokana na kuongezeka Waislamu Canada ambao ni milioni 1.5 na idadi hiyo inakadiriwa kuongekeza kwa asilimia 13 kila mwaka.

Uchumi 'Halal' umejengeka katika msingi wa mahitajio ya Waislamu zaidi ya bilioni 2 duniani ambao wanataka bidhaa na huduma ambazo zinaenda sambamba na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Ili kuzalisha bidhaa au kutoa huduma halali si lazima mwenye kufanya hivyo awe Mwislamu.

Uchumi 'Halal' duniani unakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya   dola trilioni  3 na umetajwa kuwa sekta inayokuwa kwa kasi zaidi duniani.

4055783

Kishikizo: canada ، halal
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: