IQNA

Orodha ya maeneo yenye bidhaa na huduma Halal mjini New York

9:12 - May 16, 2022
Habari ID: 3475256
TEHRAN (IQNA)- Orodha ya maeneo yenye huudma na bidhaa Halal katika mji wa New York, Marekani imechapishwa kwa lengo la kuwasaidia wenyeji na watalii Waislamu katika jiji hilo ambalo ni makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Shirika la NYC & Company ambalo ni shirika ramsi la mauzo na mikutano katika wilaya tano jijini New York limechapisha kijitabu kujulikanacho kama  "Halal Travel Guide". Hii ni mara ya kwanza orodha kama hiyo kuchapishwa na shirika la utalii Marekani na inalenga kuarifisha maeneo yenye huduma na bidhaa  Halal hasa migahawa.

Fred Dixon Mkurugenzi wa NYC & Company amesema Waislamu wamekuwa katika jamii ya New York kwa muda wa karibu miaka 400 na hivyo orodha hiyo inalenga kuonyesha bidhaa Halal katika wilaya zote za mji huo.

Kuna zaidi ya misikiti 275 katika wilaya zote tano za New York na idadi hiyo ni kubwa zaidi ya miji yote ya Marekani. Kwa mfano eneo la Brooklyn lina Waislamu kutoka mabara yote ya dunia na mbali na msikiti wa kihistoria pia kuna kumbi kadhaa za sala, migahawa na hoteli zenye kutoa huduma "Halal".

Kati ya migahawa iliyo katika orodha hiyo ni Eatzy Thai eneo la Queens, Junoon huko Manhattan, Al Aqsa eneo la Bronx, Al Humza Restaurant katika Kisiwa cha Staten na Bagel Point huko Brooklyn.

Miongoni mwa hoteli zinazotoa huduma Halal ni Conrad New York Midtown, Lotte New York Palace, The Plaza Hotel and more.

Maelezo zaidi yanapatikana katika tovuti ya  nycgo.com/HalalTravelGuide

3478916

Kishikizo: halal ، new york ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :