IQNA

Afrika inaweza kunufaika na sekta ya ‘Halal’ duniani yenye thamani ya dola bilioni 739

20:10 - October 07, 2021
Habari ID: 3474393
TEHRAN (IQNA)- Afisa mmoja wa ngazi za juu nchini Malaysia amesedma nchi za Afrika zinaweza kunufaika na soko kubwa la sekta ya chakula ‘Halal’ duniani yenye thamani ya dola bilioni 739.

Naibu Mkurugenzi wa  Taasisi ya Kilimo cha Kitropiki na Usalama wa Chakula katika Chuo kikuu cha  Putra nchini Malaysia Dkt. Awis Sazili ambaye amesema sekta ya chakula Halal duniani itafika dola billlioni 739.59 ifikapo mwaka 2025.

Amesema nchi za Afrika zinaweza kustawi kiuchumi kwa kutumia fursa zitokanazo na sketa ya chakula Halal duniani.

Dkt. Sazili ameyasema hayo katika Kikao cha Intaneti cha Sekta ya Halal Nigaria ambayo kimehudhuriwa na washiriki kutoka nchi kama vile Malaysia, Bangladesh, Pakistan na New Zealand.

Akizungumza katika kikao hicho,Dkt Abdullahi Shuaib, mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Jaiz  ya Vyeti vya Halal amebainisha masikitiko yake kuwa Waislamu Nigeria hawajatumia fursa zilizopo katika sekta ya bidhaa Halal ikilinganishwa na Waislamu waliowachache katika nchi kama vile Australia na New Zealand.

Dkt. Shuaib ametoa wito kwa mashirika ya Kiislamu kuwaelimisha Waislamu kuhusu bidhaa halali na fursa za kibiashara zilizopo katika sekta hii.

Vyakula ‘Halal’ ni vile ambavyo hutayarishwa kikamilifu kwa kuzingatia mafundisho ya Kiislamu na mfano maarufu wa hilo ni nyama ambazo huchinjwa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.

4002978

Kishikizo: halal waislamu afrika
captcha