TEHRAN (IQNA) – ‘Wiki ya Halal’ imeandaliwa kwa mara ya kwanza huko Taiwan kwa lengo la kuarifisha bidhaa na huduma ambazo zimetayarishwa kwa kuzingatia mafundisho ya Kiislamu.

Baraza la Ustawi wa Biashara ya Kimataifa Taiwan (TAITRA) limeandaa ‘Wiki ya Halal’ kwa njia ya intaneti ambapo washiriki wameweza kufanya vikao na kuonyesha bidhaa zao.
Katika maonyesho hayo, bidhaa 60 ‘Halal’ ambazo zimetengenezwa Taiwan zimeonyeshwa ambapo mashirika zaidi ya 400 yameweza kuonyeshwa bidhaa hizo. Washiriki walikuwa ni kutoka nchi kama vile Indonesia, Malaysia, Ufilipino, Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi kadhaa za Afrika.

Waandalizi wa mjumuiko huo wamesema maeonyesho hayo yataendelea hadi mwisho wa mwezi wa Oktoba kwa njia ya intaneti kwa kubonyeza hapa.