IQNA

Rais wa Iraq: Mashahidi Soleimani, Al Muhandis walichangia pakubwa vita dhidi ya magaidi

17:28 - January 05, 2022
Habari ID: 3474769
TEHRAN (IQNA)- Rais Barham Salih wa Iraq amesema mashahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis walikuwa na nafasi muhimu sana katika vita dhidi ya magaidi nchini humo hasa magaidi wa ISIS au Daesh.

Rais Salih ameyasema hayo Jumatano mjini Baghdad wakati wa kumbukumbu ya mwaka wa pili wa kuuawa shahidi makamanda hao wawili na kuongeza kuwa, Luteni Jenerali Soleimani alikimbia kuwasiadia watu wa Iraq na alifanikiwa kuikoa nchi hiyo kutoka magaidi wa ISIS.

Akizungumza katika kikao hicho mkuu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi (PMU) Falah Al Fayyad amesema PMU itaendelea kushirikiana na serikali ya Iraq ili kuhakikisha wanajeshi vamizi wa Marekani wanaondoka nchini humo.

Ikumbukwe kuwa, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi (PMU) na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi vamizi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Hujuma hiyo ilitekelezwa kwa amri ya rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump.

Kufuatia jinai hiyo, mnamo Januari 8 mwaka 2020, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilichukua hatua ya kulipiza kisasi kwa kuvurumisha makombora kadhaa dhidi ya kituo cha kijeshi cha Marekani cha Ain al Assad nchin Iraq. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa bado haijamaliza kulipiza kisasi mauaji ya Shahidi Soleimani na kwamba kuondoka askari wote wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia ndiko kutalipiza kisasi damu ya Luteni Jenerali Soleimani.

4026450

captcha