IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran

Waliotekeleza mauaji ya Qassem Soleimani wataadhibiwa

19:30 - December 31, 2021
Habari ID: 3474748
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema wale walote waliotekeleza mauaji ya kigaidi dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani hatimaye wataadhibiwa.

Ayatullah Ahmad Khatami amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya kimaanawi na kisiasa ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran ambapo ameashiria kukaribia mwaka wa pili tangu kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusema kuwa, Iran iliizaba kibao Marekani kwa kushambulia kambi yake ya kijeshi ya Ain al-Asad nchini Iraq, lakini kisasi cha mwisho kitakuwa ni kuadhibiwa wale wote waliosababisha mauaji hayo, waliotekeleza na waliotoa ushauri wa kuuawa Luteni Jenerali Qassem Soleimani hususan Trump mtenja jinai ambaye alitangaza wazi kuhusika na jinai hiyo.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Hujuma hiyo ilitekelezwa kufuatia amri ya rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump.

Kwingineko katika hotuba yake ya Sala ya Ijumaa Tehran, Ayatullah Khatami amesema kuwa, kama utawala haramu wa Kizayuni wa Israel utathubutu kufanya kosa dogokabisa, vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vitatoa jibu kali dhidi yake ambalo litakuwa ni la kuumiza.

Sambamba na kuashiria manuva ya kijeshi ya hivi karibuni ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) yaliyopewa jina la Mtume Mtukufu SAW-17 na radiamali ya viongozi wa Israel kwa manuva hayo ya kijeshi Ayatullah Khatami amesema kuwa, sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni za kujihami na za kumfanya adui asijaribu kulishambulia kijeshi taifa hili.

Hata hivyo, Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema, kama utawala wa Kizayuni wa Israel utafanya kosa dogo kabisa na kufanya hujuma ya kijeshi dhidi ya taifa hili, basi utakabiliwa na jibu kali la makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

4024953

Kishikizo: iran khatami Soleimani irgc
captcha