IQNA

Sheikh wa Al Azhar azungumza na Mfalme wa Jordan Kuhusu Quds Tukufu

13:45 - January 20, 2022
Habari ID: 3474829
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Ahmad El Tayyib, Sheikh Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri amefanya mazungumzo ya simu na Mfalme Abdallah wa Pili wa Jordan.

Kwa mujibu wa taarifa, katika mazungumzo hayo, Sheikh El Tayyib  amelaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia kama vile kamatakamata kinyume cha sheria na kuharibiwa nyumba za Wapalestina hasa eneo la Sheikh Jarrah mjini Quds (Jerusalem) ambao unakaliwa kwa mabavu na Israel. Aidha Sheikh Mkuu wa Al Azhara amemshukuru Mfalme Abdullah II bin Al-Hussein wa Jordan kwa msomamo wake wa kuunga mkono Palestina.

Kwa upande wake Mfalme Abdullah wa Jordan amesema nchi yake inaendelea kutekeleza majukumu ya kihistoria ya kulinda maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo katika mji wa Quds.

Amesema pia kuwa Jordan inaendelea kuunga mkono watu wa Palestina huku akibainisha kuwa, hatua za Israel dhidi ya Wapalestina zinadhoofisha jitihada za kufikiwa amani adilifu.

/4029992

captcha