IQNA

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Kisasi kikali kinawasubiri waliomuua Shahidi Qasem Soleimani

20:11 - January 07, 2022
Habari ID: 3474776
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu imetangaza kuwa, kutimuliwa utawala wa Marekani katika eneo nyeti la Asia Magharibi ni jibu kwa ujuha na ujinga wa adui katika kumuua Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu iliyotolewa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani imesisitiza kwamba, kisasi kikali ni kitu kisichotenganishika kabisa na faili la shahidi huyu na ni chaguo ambalo litaendelea kuwa katika meza ya taifa la Iran mpaka siku yenyewe itakapowadia.

Tarehe 3 Januari 2020 serikali ya Marekani ilimuua Luteni Jenerali Qasem Soleimani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mji mkuu wa Iraq pamoja na baadhi ya wasaidizi wake, akiwemo Abu Mahdi al-Mohandis, Naibu Mkuu wa harakati ya wananchi wa Iraq ya al Hashdu al Shaabi. Mauaji hayo ya kinyama yalifanyika kwa agizo la Donald Trump Rais wa wakati huo wa Marekani.

Kufuatia mauaji hayo ya kigaidi, tarehe 8 Januari yaani siku tano baada ya tukio hilo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) lilivurumisha makombora kadhaa ya balestiki na kuilenga kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ainul-Asad katika mkoa wa al-Anbar nchini Iraq. Baada ya tukio hilo, Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon ilitangaza hatua kwa hatua kwamba, askari wake 110 waliokuwa katika kambi hiyo walijeruhiwa na kupata madhara ya ubongo na hivyo kuwa chini ya uangalizi wa kitiba. 

665400

captcha