IQNA

Mabango ya Shahidi Soleimani katika Ukanda wa Ghaza

20:30 - January 02, 2022
Habari ID: 3474755
TEHRAN (IQNA)-Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza wamepamba mitaa yao kwa mabango makubwa ya Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Mabango hayo yamewekwa katika wakati huu wa mkesha wa kukumbuka kuuawa shahidi Kamanda Soleimani na wanajihadi wenzake.

Muhammad al Buraim, mkurugenzi wa habari katika Kamati za Muqawama za Wananchi wa Palestina amesema Wapalestina wanachukua fursa ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Qassem Soleimani kutangaza kuwa wataendeleza harakati za za muqawama au mapambano .

Amesema harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina zitaendeleza  nji ya ukombozi wa Quds ambayo ni njia iliyokuwa ikifuatwa na Shahidi Soleimani.

Al Buraim ameongeza kuwa  Palestina  kati haitasahau damu ya Shahidi Soleimani ambayo alijitolea katika kuunga mkono taifa la Palestina.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.

نصب تصاویر سردار سلیمانی در خیابان‌ها و میادین غزه
 
نصب تصاویر سردار سلیمانی در خیابان‌ها و میادین غزه


/3477194

captcha