IQNA

Misri yajitayarisha kutuma wasomaji Qur’ani nje ya nchi Ramadhani

18:55 - January 06, 2022
Habari ID: 3474774
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu ya Misri imepanga mashindano ya qiraa ya Qur’ani Tukufu kwa maqarii watakaotumwa nje ya nchi katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa miongoni mwa watakaoshiriki mashindano hayyo kuna maqarii, maimamu waadhini na wafanyakazi wa vituo vya kidini.

Awamu ya kwanza ya mashindano hayo itafanyika katika vituo vya wizara hiyo mikoani na kisha fainali itafanyika Cairo katika jengo la Wizara ya Wakfu.

Kila mwaka wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  Misri hutuma wasomaji Qur’ani na wahubiri katika nchi mbali mbali duniani.

Wamisri ni maarufu kwa usomaji Qur'ani na hadi sasa kuna wasomaji au maqarii wengi wa Qur'ani kutoka nchi hiyo ambayo wamepata umashuhuri duniani na miongoni mwa walivuma zaidi ni marhum Sheikh Abdul-Basit Abdus-Samad.

4026625

captcha