IQNA

Watoto 8 wa familia moja Misri wamehifadhi Qur'ani Tukufu

16:37 - February 24, 2021
Habari ID: 3473678
TEHRAN (IQNA) – Mohammad al-Fardi ni baba Mmisri ambaye watoto wake wote 8 wamehifadhi Qur'ani Tukufu.

Baba huyo mwenye umri wa miaka 37 anaishi katika jimbo la Sharqia na ana mabanati wanne na wavulana wanne. Watoto wote hao wanasoma katika shule ambazo zinafungamana na Chuo Kikuu cha Al Azhar.

Binti mkubwa zaidi, Mina, ni mwanafunzi wa shule ya upili na amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Rihab naye amehifadhi Qur'ani yote isipokuwa Sura al-Baqara. Hazim, ambaye ni mtoto wa tatu amehifadhi Juzuu 15 kati y azote 30 katika Qurani Tukufu. Aidha yeye ni qarii mwenye uwezo wa juu na husoma Qur;ani katika msikiti wa kijini kwake kila Ijumaa. Hazima huiga mtindo wa qarii mashuhuri wa Misri Abdul Basit Abdul Swamad katika usomaji wake.

Watoto wengine wa Muhammad wamehifadhi Juzuu kadhaa za Qur'ani Tukufu na azma hayo ni hatimaye kuweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

 

داستان زندگی 8 حافظ قرآن در یک خانواده مصری +عکس
 
داستان زندگی 8 حافظ قرآن در یک خانواده مصری +عکس
 
داستان زندگی 8 حافظ قرآن در یک خانواده مصری +عکس
 
داستان زندگی 8 حافظ قرآن در یک خانواده مصری +عکس

 

3955842

captcha