IQNA

Waislamu Uingereza

Uchunguzi: Asilimia 75 ya Waislamu wa Uingereza wanahofia usalama wao

13:47 - August 18, 2024
Habari ID: 3479295
IQNA -Kuna wasiwasi unaoongezeka miongoni mwa Waislamu wa Uingereza kuhusu usalama wao baada ya ghasia za hivi majuzi nchini humo.

Robo tatu ya Waislamu wanasema wana wasiwasi kuhusu usalama wao, kulingana na utafiti mpya – ikiwa ni ongezeko la karibu 60% tangu wiki ya machafuko ya mrengo wa kulia yaliyotokea kote nchini.

Mtandao wa Wanawake wa Kiislamu uliwahoji wanachama wake 200 kuhusu jinsi walivyohisi usalama nchini Uingereza kabla na baada ya ghasia hizo.

Kati yao 75% walisema walikuwa na wasiwasi sana kuhusu usalama wao sasa, ikilinganishwa na 16% kabla ya ghasia.

Takriban mmoja kati ya watano walisema walikumbana na uhasama tangu tukio la kuchomwa visu huko Southport, ambapo habari potofu kuhusu mshukiwa mkuu wa shambulio hilo zilizua vurugu za siku nyingi kote Uingereza.

Lila Tamea, ambaye alitafuta hifadhi katika Msikiti wa Abdullah Quilliam mjini Liverpool wakati makabiliano kati ya waandamanaji wa siasa kali za mrengo wa kulia na wapinzani yalipozuka siku ya Ijumaa Agosti 2, alisema kuwa hata kabla ya ghasia hizo alihisi kuwa hawezi kutegemea polisi kumlinda yeye na jamii yake.

Amina Atiq, mshairi mwenye umri wa miaka 29, alisema: "Nilihisi kana kwamba haikuwa sawa kwamba hatukupata nafasi kama familia ya Kiislamu kuomboleza wasichana watatu wadogo.

Baroness Shaista Gohir, mtendaji mkuu wa Mtandao wa Wanawake wa Kiislamu, ameitaka serikali kuchunguza sheria yake ya uhalifu wa chuki.

3489536

Habari zinazohusiana
captcha