IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Mwanamke Muislamu ahujumiwa katika treni London, Hijabu yake yavutwa

15:43 - February 22, 2022
Habari ID: 3474960
TEHRAN (IQNA)- Mwanamke mmoja Muislamu ameuhujumiwa akiwa ndani ya treni mjini London ambapo Hijabu yake imevutwa na mtu anayeaminikwa kuwa ni mwenye chuki dhidi ya Uislamu.

Kitengo cha Polisi katika Sekta ya Usafiri Uingereza (BTP) kimesambaza klipu ya kamera za usalama inayomuoneysha mwamake Muislamu akishambuliwa akiwa ndani ya treni aina ya DLR wakati ikikaribia kituo cha Poplar eneo la East London.

Kwa mujibu wa BTP, mwanaume mbgauzi alimshambulia mwanamke Muislamu na kujaribua kuivua Hijabu yake kisha akajaribu kumpokonya begi lake.

Polisi wanaendeleza uchunguzi na wametoa wito kwa umma kusaidia katika kumtia mbaroni mtenda jinai hiyo.

Shirika la kutetea haki za Waislamu, Tell MAMA UK limetoa wito kwa wasafiri Waislamu, hasa wanawake, kuzingatia mazingira yao wanaposafiri na kuchukua tahadhari  na ikiwezekana wachukue picha ya mshambuliaji.  

Uchunguzi wa Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu Uingereza umebaini kuwa asilimia 80 ya Waislamu Uingereza wanakabiliwa na chuki dhidi ya Uislamu.

Aidha takwimu rasmi za Uingereza zinaonyesha kuwa Waislamu ni jamii ya wachache inayokabiliwa na ubaguzi mkubwa zaidi. Takwimu zinaonyesha kuwa kuwa  ni vigumu kwa Waislamu kupata kazi ikilinganishwa na watu wa dini zingine.

4038033

captcha