IQNA

Msomi wa Qur’ani Palestina afariki akiwa na umri wa miaka 74

23:02 - January 29, 2022
Habari ID: 3474866
TEHRAN (IQNA)-Msomi maarufu wa Misri Sheikh Salah Abdul Fattah al Khaledi, msomi mwandamizi wa Palestina katika uga wa sayansi za Qurani na tafsiri amefariki dunia.

Msomi huyo amefariki Ijumaa akiwa na umri wa miaka 74. Al Khaledi alizaliwa Jenin, Palestina mwaka 1947 na alijiunga na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar mwaka 1965 na kuhitimu katika taaluma ya Sharia mwaka 1970.

Alipata Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Imam Muhammad mjini Riyadh Saudia mwaka 1977 ambapo hoja yake ya utafiti ilikuwa kuhusu mfasiri maarufu wa Qur’ani wa Misri Sayyid Qutb. Aliendeleza masomo na kupata Shahad ya Uzamivu katika chuo hicho hicho mwaka 1984 ambapo utafiti wake ulikuwa na anuani ya ‘Katika Kivuli cha Qur’ani’. Msomi huyo Mpalestina ameandika vitabu kadhaa kuhusu tafsiri ya Qur’ani Tukufu na pia kuhusu Qur’ani na kadhia ya Palestina.

4032040

captcha