IQNA

Mpalestina Aandika Kitabu kwa Wanaohifadhi Qur'ani Akiwa Gerezani Israel

21:21 - May 04, 2025
Habari ID: 3480636
IQNA-Ramadhan Mushahara, Mpalestina mwenye umri wa miaka 49, amechapisha kitabu kiitwacho “Qur'ani kwa Wanaohifadhi”. Aliandika kitabu hiki akiwa gereza za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel, licha ya vizuizi vikubwa vya gerezani.

Mushahara ametumikia kifungo cha miaka 23 katika magereza ya utawala ghasibu wa Israel."Nilikuwa gerezani kwa  miaka ishirini na tatu, maisha yalimejaa maelezo na visa vingi, lakini namshukuru Mungu kwani muda ulipita haraka. Sikupata nafasi ya kufikiria maisha nje ya gereza. Siku zangu zilijaa masomo, ufundishaji na kujifunza. Kama wavamizi wasingenichukua mateka, nisingeweza kutoka gerezani nikiwa na kitabu hiki."

Wazo la kitabu hiki lilitokana na hitaji halisi ambalo Mashahara alilipitia ndani ya familia yake. Alipoanza kuhifadhi Qur'ani pamoja na wenzake, walikumbana na changamoto kubwa kuhusu aya zinazofanana sana (Mutashabih). Hali hii ilimfanya afanye utafiti wa kina na kupitia vitabu mbalimbali hadi akapata wazo la Qur'ani maalum kwa wanaokariri. Aliendelea kuboresha wazo hili kwa miaka kumi.

Mushahara pia ameoa heshima kwa kiongozi wa zamani wa Hamas, Yahya Sinwar, aliyeuawa shahidi mwaka uliopita. Alipokuwa gerezani, Mushahara alijifunza sarufi na muundo wa Qur'ani kutoka kwa shahidi Sinwar, jambo lililomsaidia kuelewa maana ya Qur'ani kwa mtazamo tofauti.

Mushahara ana matumaini kuwa kitabu chake kitawasaidia wote wanaotaka kuhifadhi Qur'ani.

3492925

captcha