IQNA

Wapalestina 40,000 wafanikiwa kusali Sala ya Ijumaa Msikiti wa Al Aqsa

7:56 - February 05, 2022
Habari ID: 3474891
TEHRAN (IQNA)- Wapalestina wasiopungua 40,000 wameshiriki katika Sala ya Ijumaa wiki hii katika Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Palestina  lwa Wafa, Idara ya Wakfu ya Mji wa Quds imetangaza kuwa, idadi ya waumini Wapalestina waliosali Sala ya Ijumaa wiki hii katika Msikiti wa Al Aqsa ilikuwa takribani watu 40,000. Hii ni katika hali ambayo wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel walikuwa wameweka sheria kali za kuwazuia Wapalestina kufika katika msikiti huo mtakatifu kwa ajili ya Sala ya Ijumaa. Taarifa ziansema askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliwazuia maelfu ya Wapalestina kusali Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa.

Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel huwazuia Wapalestina wengi kufika katika Msikiti wa Al Aqsa wakati wa Sala ya Ijumaa.

Msikiti wa Al Aqsa umegeuzwa kuwa eneo la kutamba na kujifaragua askari wa utawala haramu wa Israel na walowezi wa Kizayuni wanaochukua hatua zinazolenga kuubadilisha utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa mji wa Quds (Jerusalem) na badala yake kuufanya kuwa na nembo za Uzayuni.

Utawala wa Kizayuni unachukua hatua hizo za kibeberu kuhusiana na mji wa Baitul Muqaddas na msikiti wa Al Aqsa wakati Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO lilipitisha azimio mwaka 2016 lililopinga kuwepo uhusiano wowote wa kihistoria, kidini au kiutamaduni kati ya Mayahudi na maeneo matakatifu ya mji wa Quds na hasa msikiti wa Al Aqsa na kusisitiza kuwa, msikiti huo ni mahala patakatifu kwa Waislamu.

Mji wa Quds ulipo msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu isiyotenganika na ardhi ya Palestina na moja ya maeneo matatu muhimu zaidi matakatifu ya Kiislamu.

4033736/

captcha