IQNA

Baraza la Fatwa Palestina lataka umma ulinde Msikiti wa Al Aqa

17:20 - February 20, 2022
Habari ID: 3474952
TEHRAN (IQNA)- Baraza Kuu la Fatwa Palestina limetoa wito kwa umma kote Palestina kujitokeza kuulinda Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Katika kikao kilichoongozwa na Sheikh Muhammad Hussein, Mufti Mkuu wa Quds, baraza hilo limelaani kukithiri vitendo vya Wazayuni maghasibu kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa na hujuma dhidi ya mtaa wa Sheikh Jarrah mjini Quds.

Taarifa hiyo imesema hujuma hizo ni sawa na maangamizi ya kimbari ya wakazi wa Sheikh Jarrah mbali na kuwa ni mbinu ya kuuyahudisha mji huo.

Baraza hilo limeonya kuwa chokochoko hizo za Wazayuni yamkini zikaibua migogoro katika eneo zima la Asia Magharibi.

Baraza Kuu la Fatwa Palestina pia limeelaani n jama za utawala wa Kizyauni wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds na Msikiti wa Nabii Ibrahim mjini Al Khalil ni milki ya Waislamu na Wazayuni hawana haki ya kuingilia usimamizi wa maeneo hayo matakatifu.

Halikadhalika baraza hilo limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kuulazimisha utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe hujuma dhidi ya Wapalestina.

4037559

captcha