Hatua hii, kwa mujibu wa taarifa, inatokana na mapendekezo ya Kamati ya Usalama ya Bunge la Israel, Knesset,.
Gavana wa al-Quds amelaani uamuzi huo, akiutaja kuwa ni kitendo cha kiholela kinachokiuka waziwazi haki ya msingi ya uhuru wa kuabudu. Amesema hatua kama hizi ni sehemu ya mpango mpana wa kuimarisha udhibiti wa mji huo na kuendelea kukanyaga haki za kidini za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza.
Ameongeza kuwa wakati huohuo, mashambulizi ya walowezi wa Kiyahudi wanaoingia kwa nguvu katika eneo la Al-Aqsa kwa ulinzi wa maafisa wa Israel yameongezeka, huku vikwazo vya umri vilivyowekwa vikiwanyima maelfu ya Wapalestina fursa ya kuingia msikitini tangu Oktoba 2023.
Aidha, utawala wa Tel Aviv uliweka mzingiro mkali kuzunguka Al-Aqsa na kuzuia kabisa Wapalestina kuufikia msikiti huo baada ya kuanzisha vita dhidi ya Gaza iliyozingirwa. Pia ulitoa amri nyingi za kuwafukuza wakazi wa al-Quds ili kuwazuia kuswali katika mwezi wa Ramadhani.
Harakati za Kiislamu za kupigania ukombozi wa Palestina zimeshutumu vikali hatua hizi, zikionya kuwa utawala huo “unacheza na moto” kwa kuendelea kukiuka utakatifu wa eneo hilo tukufu.
Habari inayohusiana:
Msikiti wa Al-Aqsa ni mahali patakatifu pa tatu kwa utukufu katika Uislamu. Wayahudi huliita eneo hilo Temple Mount, wakidai kuwa palikuwa na mahekalu mawili ya kale ya Kiyahudi.
Israel iliteka Jerusalem Mashariki (al-Quds), ambako Al-Aqsa ipo, katika vita vya Waarabu na Israel vya mwaka 1967, na baadaye ikatangaza kuunganisha mji mzima mwaka 1980, hatua ambayo haijawahi kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa.
3496068