IQNA

Facebook yakosolewa kwa misimamo dhidi ya Palestina

22:36 - February 23, 2022
Habari ID: 3474964
TEHRAN (IQNA)-Kampuni moja ya mawakili yenye makao yake makuu London imetuma barua rasmi ya malalamiko kwa Facebook kuhusu misimamo yake dhidi ya Wapalestina.

Ikielekezwa na Kituo cha Kimataifa cha Haki kwa Wapalestina (ICJP), kampuni ya mawakili ya Bindmans LLP imetaka Facebook itoe maelezo kuhusu ubadanji  mpana na wa makusudi wa  akaunti za Facebook zinazohusiana na Palestina.

Malalamiko hayo pia yalitumwa kwa Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukuzaji na ulinzi wa uhuru wa maoni na kujieleza. Malalamiko hayo yanaomba uhakiki wa haraka wa, na ufafanuzi wa maamuzi yaliyofanywa na Facebook, ambayo ilibadilishwa jina Oktoba mwaka jana na kuitwa Meta Inc, kuhusu kusimamisha akaunti na machapisho ambayo yanahusishwa na mashirika ya habari ya Palestina, wachambuzi  na waandishi wa habari.

Barua ya Jumatatu ya malalamiko kwa Facebook ni ya pili kati ya miezi tisa iliyotumwa na Bindmans LLP kwa kampuni hiyo kubwa ya mitandao ya kijamii. Mawasiliano ya awali yaliyowasilishwa Mei 2021 yalifanywa kwa niaba ya waandishi wa habari watano na mashirika ya habari nchini Palestina. Facebook inasemekana kuingilia akaunti na/au machapisho yao na ilishutumiwa kwa kukiuka haki yao ya kimsingi ya uhuru wa kujieleza pamoja na Sera yake ya Haki za Kibinadamu.

Katika malalamiko ya Mei 2021, maswali makuu yaliyoulizwa na Bindmans LLP yalijumuisha ikiwa maamuzi ya udhibiti yalifanywa na algoriti au na mtu anayetumia hiari yake, na maelezo kuhusu sera ya Facebook katika kuhalalisha maamuzi yao ya udhibiti, pamoja na hatua zilizochukuliwa na kampuni kutatua udhibiti usio wa haki.

Malalamiko yanarejesha ombi kwamba Meta/Facebook ifichue na kukagua mchakato wake wa kufanya maamuzi, na kueleza ni kwa nini akaunti zilifungwa, kusimamishwa au machapisho kuondolewa, na ikiwa kwa kufanya hivyo ilitumika algoriti au uamuzi wa kibinadamu.

Shirika la Meta/Facebook linaonekana kupendelea wazi utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umezikoloni na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

3477938/

captcha