IQNA

Waislamu Marekani

Utafiti wa hali ya Waislamu wa Marekani Wazinduliwa na CAIR

16:32 - August 24, 2023
Habari ID: 3477488
WASHINGTON, DC (IQNA) - Utafiti wa matatizo yanayowasibu Waislamu wa Marekani umezinduliwa na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR).

Utafiti huu  unaochukua  dakika moja kwa kila anayehojiwa unalenga kuangazia suala nyeti ambalo linaathiri jamii ya Kiislamu na kuchangia kukomesha ubaguzi na pia kuzuia vitendo vya serikali kuwalenga kimakosa Waislamu.

Waislamu watakaohojiwa  wana chaguo la kujaza fomu au kutumia  Kodi ya QR kuwasilisha maoni yao.

Kwa kutambua Septemba hii ijayo inaadhimisha mwaka wa 20 wa orodha ya ugaidi ya shirikisho yenye ubaguzi na iliyo kinyume cha sheria, CAIR inatoa wito kwa Waislamu wote wa Marekani kushiriki katika uchunguzi huu wa maoni, unaoendelea hadi Ijumaa, Septemba 15.

CAIR inabainisha kuwa majibu yote ya utafiti yatakuwa siri na hivyo waliojaza hawatajulikana.

Utafiti huu wa Waislamu wa Marekani unalenga kuangazia ukweli kuhusu ukweli kwani ripoti ya hivi majuzi ya CAIR ilipata asilimia 98 ya majina milioni 1.47 kwenye nakala iliyovuja ya orodha ya washukiwa wanaochunguzwa ya 2019 ni ya Waislamu.

Kuwa katika orodha hiyo huwa na athari mbaya kwani mashirika ya serikali huitumia kuwanyanyasa na kuwadhalilisha watu wakati wa safari zao, kuwakataza moja kwa moja kutumia ndege, kunyima leseni na vibali, kuzuiwa kupata ajira au kusitisha kazi zilizopo, na hata kuchelewesha au kukataa visa na maombi ya uraia wa Marekani au pasipoti ya Marekani.

"Maarifa ya jumuiya ya Kiislamu kupitia utafiti huu yatachangia uelewa wa kina wa suala hili na uwezekano wa kuleta mabadiliko ya maana au mageuzi kamili," alisema Mkurugenzi wa CAIR wa Idara ya Masuala ya Serikali Robert S. McCaw.

"CAIR inaamini kwamba kila sauti ni muhimu, na uchunguzi huu unawawezesha Waislamu wa Marekani kushiriki uzoefu wao, changamoto, na wasiwasi wao kuhusiana na mfumo wa ufuatiliaji."

3484913

Habari zinazohusiana
Kishikizo: waislamu cair
captcha