IQNA

10:44 - March 06, 2022
Habari ID: 3475014
TEHRAN (IQNA) - Katika taarifa yake, jopo la majaji limepongeza kiwango cha hali ya juu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya mwaka huu nchini Iran.

Duru ya 38 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran pamoja na mashindano ya kimataifa ya wanawake, wenye ulemavu wa macho na wanafunzi wa shule yalimalizika Jumamosi mjini Tehran baada ya washindi wa kila kategoria kupokea tuzo zao.

Jopo la waamuzi, linalojumuisha wataalam kutoka Iran, Iraq, Pakistan, Afghanistan, Jordan, na Morocco walitoa taarifa mwishoni mwa mashindano hayo

Ilianza kauli hiyo kwa Aya ya 92 ya Surah Al-Anbiya isemayo “[Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi ."

Ujumbe wa wataalamu wa Qur'ani wa Umma wa Kiislamu katika mashindano hayo ni ule wa umoja wa amani kwa kushikamana na Qur'ani Tukufu kama kipengele cha kuunganisha, imesema taarifa hiyo..

"Tunapongeza kiwango cha hali ya juu cha usomaji katika toleo hili na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo," ilibainisha taarifa, na kuongeza kuwa uwanja unapaswa kuwekwa kwa ajili ya kukuza Qur'ani katika kizazi kipya duniani kote ili kujenga "Umma Moja wa Qur'ani”.

Jopo hilo pia limepongeza juhudi za waandalizi wa mashindano ya mwaka pamoja na vyombo vya habari kwa kuangazia tukio hilo.

4040479

Kishikizo: mashindano ya qurani ، iran
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: