IQNA

Zaidi ya Waislamu 100 Warohingya wawasili Ufukwe wa Indonesia baada ya wiki kadhaa baharini

17:05 - March 07, 2022
Habari ID: 3475019
TEHRAN (IQNA)- Zaidi ya Waislamu 100 wa jamii ya Rohingya waliokuwa na njaa na udhaifu mkubwa wa kimwili walipatikana kwenye ufuo wa bahari katika mkoa wa kaskazini mwa Indonesia wa Aceh baada ya wiki kadhaa baharini.

Kundi hilo lilifika kwenye ufuo wa Jangka karibu na Alue Buya Pasi, kijiji cha wavuvi katika wilaya ya Bireuen, kwa mashua ya mbao iliyochakaa mapema Jumapili, wamesema maafisa wa serikali eneo hilo.

Wanakijiji ambao waliona kabila Warohingya hao waliwasaidia kutua na kisha kuripoti kuwasili kwao kwa mamlaka, alisema Badruddin Yunus, kiongozi wa jumuiya ya kikabila ya wavuvi.

"Wanaonekana dhaifu sana kutokana na njaa na upungufu wa maji mwilini baada ya safari ndefu na kali baharini," Yunus alisema, akiongeza haijulikani ni wapi kundi hilo lilikuwa likisafiri kutoka au lilikoelekea kwani hakuna aliyezungumza Kiingereza au Kimalai.

Wanaume 58, wanawake 21 na watoto 35 walipewa makazi na kupokea msaada kutoka kwa wanakijiji, polisi na wanajeshi, wakati viongozi wa eneo hilo pamoja na kikosi kazi cha coronavirus walikuwa wakisaidia kuwashughulikia, Yunus alisema.

Zaidi ya Waislamu 700,000 wa Rohingya wamekimbia kutoka Myanmar nchi yenye Mabudha wengi na kuelekea katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh tangu Agosti 2017. Waislamu Warohingya walianza kutoroka Myanmar wakati jeshi lilipoanzisha operesheni ya kuwaondoa watu waliotajwa kuwa ni waasi.

Vikosi vya usalama vya Myanmar vimeshutumiwa kwa ubakaji mkubwa, mauaji ya kimbari na kuchoma maelfu ya nyumba.

Makundi ya Warohingya yamejaribu kuondoka kwenye kambi zilizojaa watu nchini Bangladesh na kusafiri kwa bahari katika safari za hatari hadi nchi nyingine zenye Waislamu wengi katika eneo hilo.

Malaysia yenye Waislamu wengi imekuwa sehemu ya kawaida ya boti hizo, na wasafirishaji haramu wamewaahidi wakimbizi hao maisha bora huko. Lakini wakimbizi wengi wa Rohingya wanaotua Malaysia wanawek wa kizuizini.

Ingawa Indonesia haijatia saini Mkataba wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa wa 1951, UNHCR ilisema kuwa kanuni ya rais ya 2016 inatoa mfumo wa kisheria wa kitaifa unaosimamia misaada kwa wakimbizi.

3478062/

Kishikizo: rohingya waislamu
captcha