IQNA

Mapatano ya Bangladesh na UN kuhusu wakimbizi Warohingya

11:57 - October 10, 2021
Habari ID: 3474407
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umetia saini mapatano na Bangladesh kuhusu kuwasiadia wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya ambao wako katika kisiwa kimoka cha Ghuba ya Bengal.

Serikali ya Bangladesh imewahamishia wakimbizi 19,000 Warohingya hadi Kisiwa cha Bhasan Char pamoja na kuwa wakimbizi na watetezi wa haki za binadamu wanapinga hatua hiyo kwa sababu kisiwa hiicho hukumbwa na mafuriko na upepo mkali.

Itakumbukwa kuwa wimbi jipya la mauaji, mashambulizi na ubakaji wa jeshi la Myanmar katika mkoa wa Rakhine kuwalenga Waislamu wa Rohingya, lilianza tarehe 25 Agosti mwaka 2017 ambapo zaidi ya Waislamu elfu sita waliuawa na wengine elfu nane kujeruhiwa. Aidha zaidi ya Waislamu wengine milioni moja wa jamii hiyo walilazimika kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh huku wengine wakipata hifadhi katika nchi kama vile India, Thailand na Malaysia.

Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein aliesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

Mwezi Januari mwaka huu, Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) iliitaka serikali ya Myanmar kuchukua hatua za dharura za kuzuia mauaji ya kimbari ya Waislamu wa Rohingya, ikisisitiza kuwa Warohingya hao wamesababishiwa machungu na maumivu yasiyoweza kufutika au kurekebishika.

3475960

captcha