IQNA

Utawala wa Israel umewaua shahidi Wapalestina watatu

0:04 - April 03, 2022
Habari ID: 3475090
TEHRAN (IQNA) - Jeshi katili la utawala haramu wa Israel limewaua shahidi Wapalestina watatu kwa kuwapiga risasi katika mji wa Jenin, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wapalestina hao wameuawa shahidi alfajiri ya leo baada ya gari lililokuwa limewabeba kumiminiwa risasi na wanajeshi wa Israel, karibu na lango la kuingia mji wa Arraba, kusini magharibi mwa Jenin.

Jeshi katili la utawala haramu wa Israel limewaua shahidi Wapalestina hao katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Baadhi ya nchi zimeanza kutekeleza ibada ya Swaum ya Ramadhani hii leo, huku nyingine zikitazamiwa kuanza kesho Jumapili.

Utawala wa Kizayuni wa Israel mbali na kuwaua shahidi Wapalestina hao, lakini pia limezuilia gari lao, sambamba na kukataa kuzipa familia miili ya mashahidi hao kwa ajili ya kuzikwa.

Katika siku za hivi karibuni, ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu imeshuhudia operesheni kadhaa za kujitolea mhanga ambapo Wazayuni 11 wameuawa.

4046106

captcha