IQNA

Hamas na Jihad ya Kiislamu zalaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina hasa mwanamke

18:21 - April 11, 2022
Habari ID: 3475114
TEHRAN (IQNA)- Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina za Hamas na Jihad ya Kiislamu zimelaani vikali jinai za hivi karibuni za wanajeshi wa utawala haramu wa Israel ambao wamewaua Wapalestina akiwemo mwanamke.

Harakati ya Jihad ya Kiislamu imetoa taarifa na kulaani vikali mauaji hayo ambayo yametekelezwa dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na kusema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel sasa umevuja mstari mwekundu baada ya kuwua raia hasa mwanamke.

Jihad ya Kiislamu imesema adui Mzayuni ameonyesha uso wake mchafu hasa utumizi wa ugaidi kufikia malengo yake haramu.  Aidha Jihad ya Kiislamu imetoa wito kwa Wapalestina wote kusimama kidete katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakati huo huo, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameeleza kuwa moto wa mapambano dhidi ya Wazayuni unapaswa kukolezwa katika eneo lote la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Ni baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuzidisha mashinikizo na jinai zake dhidi ya Wapalestina sambamba na kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, jambo ambalo limepelekea kuongezeka mapambano ya Wapalestina na operesheni za kujitolea kufa shahidi.

Fawzi Barhoum, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, amesema leo Jumatatu kwamba harakati hiyo inawategemea mashujaa wa Ukingo wa Magharibi kwa ajili ya kulisaidia eneo la Jenin.

Barhoum ameongeza kuwa: "Operesheni za wanamapambano wa Palestina zilizofanywa na mashujaa kama Zia Hamarsheh na Raad Hazem zinapaswa kuwatia moyo vijana katika Ukingo wa Magharibi."Palestina

Msemaji wa Hamas amesema kuwa, operesheni za muqawama ni wajibu wa kidini na kitaifa na kwamba yeyote mwenye silaha anapaswa kufungua medani mpya katika mapambano dhidi ya adui Mzayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Amesisitiza kuwa hatua hiyo ni jibu halisi la Wapalestina kwa jinai zinazofanywa na Wazayuni maghasibu.

Jana asubuhi (Jumapili, Aprili 10), wanajeshi wa Israel walishambulia miji na vijiji kadhaa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, vikiwemo Jenin, Nablus, Tulkarm na Jeriko na kuwafyatulia risasi raia wa maeneo hayo. Wapalestika watatu akiwemo Ghada Ibrahim Sabatin, 47, mama wa watoto sita, wameuwa shahidi katika mashambulizi hayo ya wanajeshi wa Israel yaliyopamba moto sambamba na kuanza mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

4048358

captcha