IQNA

Matumizi ya 'Inshallah' miongoni mwa Waislamu

11:12 - May 08, 2022
Habari ID: 3475221
TEHRAN (IQNA)-Utumizi wa neno 'Insallah' (Mungu Akipenda) umeenea sana miongoni mwa Waislamu kote duniani.

Waumini hawatendi chochote bila kumkumbuka Mwenyezi Mungu na wanaamini kuwa iwapo hawatamki 'Inshallah' wakati wanapopanga kazi za mustakbali basi kazi hizo hazitofanikiwa.

Itikadi hii inatokana na aya za 23 na 24 za Sura Al Kahf ambazo zinasema

وَلَا تَقُولَنَّ لِشَيْءٍ إِنِّي فَاعِلٌ ذَٰلِكَ غَدًا ‎﴿٢٣﴾‏ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ ۚ وَاذْكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلْ عَسَىٰ أَن يَهْدِيَنِ رَبِّي لِأَقْرَبَ مِنْ هَٰذَا رَشَدًا ﴿٢٤﴾

Wala usiseme kamwe kwa jambo lolote lile: Hakika nitalifanya hilo kesho 

Isipo kuwa Mwenyezi Mungu akipenda. Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unapo sahau, na sema: Asaa Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uwongozi ulio karibu zaidi kuliko huu.

Kwa msingi huo kutamka Inshallah ni muongozo wa moja kwa moja kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa kutamka Inshallah, tunasisitiza kuwa, kazi zote zinafanyika kwa irada na uwezo wake Mwenyezi Mungu.

Aya hizi tukufu hazimaanishi kupuuza irada na uwezo wa mtu binafsi bali zinaonyesha uzingatiaji adabu na nidhamu mbele ya Mwenyezi Mungu na pia ni ishara ya kutilia maanani hali zilizo nje ya udhibiti wa mwanadamu katika kufanikisha jambo.

Katika tafsiri maarufu ya Qur'ani Tukufu ijulikanayo kama Tafsir al Mizan, aya hizo mbili hapo juu zimefasiriwa ifuatavyo: Aya hizi mbili zinataka kueleza ukweli kwamba kila kitu kilichomo duniani kiko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na Anabadilisha Apendavyo ndani yake na hakuna mwenye kumiliki chochote isipokuwa Mungu Amemiliki kitu.

Maana ya sehemu hii ya Aya isemayo: 'Wala usisema kamwe kwa jambo lolote lile: Hakika nitalifanya hilo kesho' 

 وَلا تَقُلَنَّ لِشَيْ ءٍ نِنِّي فعِعلٌ ذلِكَ غَدا

haimaanishi kuwa usijinasibishe na kazi zako, bali inasema unapokusudia kufanya jambo katika siku zijazo, kwa kusema maneno Inshallah unamaanisha kuwa utafanya kulingana na mapenzi na utaratibu wa Mungu.

Bila shaka, kusema Inshallah sio amri na usiposema hupati dhambi, lakini matumizi yake yanaonyesha dhahiri ya kumcha Mungu katika kauli ya mtamkaji.

Inafaa kuashririkia hapa kuwa Al-Mizan Fi Tafsir Al-Quran, inayojulikana zaidi kama Tafsir Al-Mizan, ni mojawapo ya tafsiri pana na za kina zaidi za Qur'ani kwa lugha ya Kiarabu na imeandikwa na Sayyid Mohammad Hussein Tabatabai (1892-1982), mwanazuoni wa Kiislamu na mfasiri wa Qur'ani wa madhehebu ya Shia.

 

captcha