IQNA

Waislamu Canada

Maonyesho ya Sanaa ya Kiislamu yazinduliwa Victoria nchini Canada

20:26 - July 30, 2022
Habari ID: 3475560
TEHRAN (IQNA) – Maonyesho ya sanaa ya Kiislamu yalizinduliwa mapema wiki hii huko Saanich, Victoria nchini Canada.

Umati ulikusanyika nje ya Ukumbi wa Manispaa ya Saanich mnamo Julai 27 kwa ajili ya ufunguzi wa maonyesho hayo.

Yameandaliwa kwa ushirikiano na Voices for Muslim Women (Sauti za Wanawake Waislamu)  ambalo ni shirika linalofanya kazi kikamilifu kushughulikia ubaguzi wa rangi na ubaguzi kwa kuunda fursa za elimu ya kitamaduni na kujieleza. Maonyesho hayo yaliyopewa jina la Al-Fatiha yamekuwa yakiandaliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika kuandaa na yanalenga kukuza hisia za kujiamini miongoni mwa Waislamu wanaoishi eneo lote la Greater Victoria.

"Maonyesho hayo yanaitwa Al-Fatiha ambayo ni sura ya kwanza katika Qur’ani Tukufu, ikimaanisha ufunguzi," mratibu Asiyah Robinson alisema. "Tunachukua njia hizo mbili. Inafungua umma kwa michango ya Waislamu katika sanaa, lakini pia tunatumai maonyesho haya sio ya mwisho ya aina yake. Tunataka kuanzisha mazungumzo ambayo ni ya wazi . Nadhani hiyo ndiyo nia ya kweli.”

Ni sehemu moja tu ya juhudi kubwa ya kuunda nafasi zaidi jumuishi kwa jamii Waislamu ambayo ni moja ya jamii zinazokuwa zaidi Canada.

 Robinson, pamoja na Zaheera Jinnah na wenzake, walitoa wito kwa mameya wa Saanich na Victoria kutekeleza mapendekezo ya kusaidia kukabiliana na suala linalokua la chuki dhidi ya Uislamu. Mapendekezo haya yanahusu sekta kadhaa, kutoka kwa mapendekezo kuhusu mageuzi ya polisi hadi ufadhili zaidi wa sanaa.

Maonyesho hayo yanaonyesha kazi za sanaa zilizoundwa na wanawake wa Kiislamu kutoka katika jimbo hilo na huchunguza mada muhimu ndani ya mila za Kiislamu na desturi za Kiislamu kama vile sala, utambulisho, uthabiti, hali ya kiroho na mwanzo mpya.

Lakini sio tu kwa wale wanaofuata Uislamu au kujitambulisha kuwa Waislamu, wanasema Robinson na Jinnah, ambao waliwaalika washiriki katika jumuiya mbalimbali za kidini kushiriki. Ni kwa jamii nzima, haswa wale ambao ni wa vikundi vingine vilivyotengwa na wenye uwakilishi mdogo, walisema.

"Tunataka kuhakikisha kuwa maonyesho haya yanajumuisha wote  na yako wazi kwa kila mtu. Hatutaki Waislamu tu wajione katika maonyesho haya, bali watu wengine, jumuiya nyingine na makundi mengine,” Robinson alisema.

Maonyesho yataendelea hadi Septemba 5.

3479888

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha