IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Ongezeko la 1300% la Matukio ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Canada

11:19 - June 07, 2024
Habari ID: 3478943
IQNA - Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Canada (NCCM) limeripoti kuongezeka kwa 1300% kwa matukio ya chuki dhidi  ya Uislamu (Islamophobia) katika nchi hiyo ya Amerika Kaskazini kufuatia kuanza kwa mauaji ya kimbari ya Isarel dhidi ya Wapalestina huko  huko Gaza.

Wabunge katika kamati inayochunguza chuki dhidi ya Uislamu na chuki dhidi ya Wayahudi walisikia Alhamisi kwamba Waislamu wengi wameuawa katika mashambulizi ya makusudi nchini Canada (Kanada) katika kipindi cha miaka saba iliyopita kuliko nchi nyingine yoyote ya kundi la G7 la nchi zilizostawi kiviwanda, na kwamba chuki dhidi ya Uislamu imeongezeka kwa kasi tangu kuanza kwa vita vya Israel dhidi ya Gaza Oktoba mwaka jana.

Akitoa ushahidi mbele ya kamati ya haki ya Bunge la Commons, Stephen Brown, mtendaji mkuu wa Baraza la Taifa la Waislamu wa Kanada (NCCM), aliongeza kuwa chuki dhidi ya Uislamu ni "aina hatari ya jinai" ambayo imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

Kamati hiyo pia ilisikia kwamba algoriti za mitandao ya kijamii zinakuza maudhui dhidi ya Uislamu, na  chuki hizo hueneza katika jamii halisia.

Bw. Brown alisema jumuiya za Waislamu zinakabiliwa na chuki na vurugu zisizo na kifani "kutoka kila ngazi ya jamii."

Bw. Brown alikuwa akizungumza katika kumbukumbu ya mwaka wa tatu wa shambulio la kigaidi mnamo Juni 6, 2021 huko London, Ontario., wakati mzungu Mkristo mwenye chuki dhidi ya Uislamu alipoendesha gari lake la mizigo kugonga familia ya Kiislamu kwa makusudi, na kuwaua wanne kati yao na kumwacha mvulana mdogo yatima.

"Katika maeneo yetu matakatifu ya ibada, na katika maeneo ya umma, Waislamu nchini Canada hawako salama kutokana na chuki dhidi ya Uislamu," alisema, akitoa mfano wa shambulio la msikiti wa Quebec City mnamo 2017 wakati mtu mwenye bunduki alipofyatua risasi katika Kituo cha Utamaduni cha Kiislamu, na kuua waumini sita na kuwajeruhi vibaya wengine watano baada ya sala ya jioni.

Bw. Brown aliiambia kamati ya Commons inayochunguza chuki dhidi ya Uislamu na chuki dhidi ya Wayahudi kwamba kabla ya shambulizi hilo, msikiti wa jiji la Quebec ulikuwa ukilengwa mara kwa mara, lakini mamlaka "haijafanya lolote."

Kichwa cha nguruwe aliyekufa kiliwekwa mbele ya msikiti, na maandamano ya Wakristo wazungu wenye misimamo mikali yaliandaliwa katika kitongoji hicho kupinga Waislamu, alisema.

Aliishutumu serikali ya Quebec kwa "kuhalalisha ubaguzi" kupitia sheria ya mkoa ambayo inakataza watumishi wengi wa umma kuvaa kile kinachotajwa kuwa ni alama za kidini, zikiwemo hijabu, kazini.

"Katika miezi michache iliyopita, kumekuwa na ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa rangi dhidi ya Wapalestina kote Canada," alisema. "Katika robo ya nne ya mwaka jana, idadi ya matukio ya chuki kama haya nchini Canada yaliyoripotiwa kwetu ambalo kulikuwa na ongezeko la asilimia 1,300," mkuu wa NCCM alisema.

Alisema wataalamu wamepoteza kazi zao au wameadhibiwa baada ya kutoa wito wa kusitishwa kwa mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel Gaza, huku wanawake wa Kiislamu waliovalia hijabu wakishambuliwa na kunyanyaswa katika maeneo ya umma.

Siku chache zilizopita, mwanamke aliyevalia hijabu huko Ottawa ambaye alikuwa akiandamana kwa amani alipigwa na magenge ya watu wenye chuki kupelekwa hospitalini kwa majeraha, aliwaambia wabunge.

3488649

Habari zinazohusiana
captcha