IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Hatua za kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu Canada

16:57 - August 07, 2022
Habari ID: 3475591
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wengi wameuawa katika mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Canada (Kanada) kuliko nchi nyingine yoyote ya kundi la G-7 kati ya 2017-2021.

Ukweli huo ulibainika nje ya Msikiti wa mji wa  London katika jimbo la Ontario, Canada mnamo Juni 8, 2021, wakati maelfu ya wakaazi wa jiji hilo na watu kutoka sehemu tofauti za nchi walipokusanyika baada ya shambulio lililopelekea Waislamu wanne kupoteza maisha katika hujuma ya kutisha ya wenye chuki dhidi ya Uislamu.

Jumuiya ya Waislamu wa London, Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Canada (NCCM), na mamia ya mashirika kote Canada waliungana kutoa wito kwa ngazi zote za serikali kuchukua hatua kushughulikia madhara ya chuki ya Uislamu.

Serikali ya shirikisho iliitikia mwito huo na ikaitisha Mkutano wa Kitaifa wa Hatua kuhusu Chuki dhidi ya Uislamu mnamo Julai 22, 2021. Mashirika ya Kiislamu kutoka British Columbia hadi Maritimes yanayowakilisha sauti mbalimbali yaliwasilisha mapendekezo ya kuchukuliwa hatua katika mkutano huo ambao ulifanyika kwa saa kadhaa. Viongozi wa Kiislamu walikutana na Waziri Mkuu Justin Trudeau, mawaziri kadhaa wakiwemo mawaziri wa Sheria, Usalama wa Umma, Turathi na wengineo.

NCCM iliwasilisha mapendekezo 61 ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu ambayo si tu kuwa inachochoewa na watu wa kawaida bali pia chuki hiyo inaonekana imeratibiwa kimfumo.

Jumla ya mapendekezo 35 ya kuchukuliwa hatua yalielekezwa kwa serikali ya shirikisho, mapendekezo 19 yalielekezwa kwa serikali za mikoa, na mapendekezo 7 yalielekezwa kwa serikali za manispaa na mikoa.

Ripoti ya Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Canada ya uwajibikaji ya mwaka mmoja inaonyesha ni serikali gani kote nchini zimejitolea au kupitisha mapendekezo mbalimbali. Ingawa mengi yamefanywa, mengi zaidi yamesalia.

Baraza hilo linasisitiza kuwa  chuki dhidi ya Uislamu imesbabisha vifo na hivyo ni wakati wa hatua zaidi, sio maneno tu katika kukabiliana na chuki hiyo.

4075951

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha