IQNA

Umaarufu wa vyakula ‘Halal’ waongezeka Russia

14:33 - February 20, 2022
Habari ID: 3474951
TEHRAN (IQNA)- Bidhaa ‘Halal’ na hasa vyakula vinazidi kupata umaarufu nchini Russsia, nchi kubwa zaidi duniani.

Kwa mujibu wa taarifa, idadi ya migahawa na taasisi ambazo zinajishughulisha katika sekta ya Halal nchini  Russia inazidi kuongezeka na bidhaa hizo hazitumiwi tu na Waislamu bali hata wasiokuwa Waislamu.

Bidhaa ‘Halal’ hutayarishwa kwa kuzingatia mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.

Wakati ambao kulikuwa na maduka mawili tuu makubwa ya bidhaa ‘Halal’ katika mjhi mkuu wa Russia, Moscow, idadi hiyo imeongezeka  sana na sasa hata katika masoko makubwa kuna vitengo maalumu vya bidhaa ‘Halal’.

Jukumu la kusimamia viwango vya bidhaa Halal liko mikononi mwa Kituo cha Bidhaa Halal katika Baraza la Mufti wa Russia. Kituo hicho baada ya kubaini bidhaa zinazalishwa kwa mujibu wa mafundishi ya Kiislamu hutoa cheti cha ‘Halal’ .

Bidhaa za Halal zinazozalishwa nchini Russia pia huuzwa katika nchi jirani zilizowahi kuwa katika Shirikisho la Sovieti ambazo zina idadi kubwa ya Waislamu.

Russia ni nchi kubwa yenye idadi ya watu takribani milioni 150 na idadi ya Waislamu nchini humo inakadriwa kuwa milioni 25.

4037307

Kishikizo: russia halal waislamu
captcha