Waandaaji wanatarajia wageni zaidi ya 20,000.
Tamasha la Kimataifa la Chakula Halal litafanyika kuanzia Septemba 28-29 kwenye Uwanja wa London Stadium, likionyesha aina mbalimbali za vyakula kutoka duniani kote.
Sekta ya Halal inahusiana an utoaji wa huduma na bidhaa kwa mujibu wa mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu. Kwa mfano nyama lazima iwe imechinjwa kwa mujibu wa mafundisho wa Kiislamu na pia iwe imetayarishwa katika eneo ambalo haichanganyiki na nyama zingine ambazo ni haramu kama vile nyama ya nguruwe au nyama ambazo hazijachinjwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.
Tamasha la Kimataifa la Chakula Halal lina orodha iliyochaguliwa kwa uangalifu ya wachuuzi, wapishi na maduka ya chakula yanayowakilisha nchi kama vile Pakistan, Uturuki, Morocco na Indonesia, miongoni mwa wengine.
Mkurugenzi wa hafla hiyo, Waleed Jahangir ameliambia gazeti la Arab News, amesema kuna ongezeko la mahitaji ya bidhaa zilizoidhinishwa kuwa ni Halal huku idadi ya Waislamu duniani ikiendelea kupanuka.
Tamasha limepanua matoleo yake ya kifamilia na eneo la watoto lililopanuliwa na bazaar. Pia imeshirikiana na Our Future Health kutoa kliniki inayohamishika ya afya, kuwapa waliohudhuria fursa ya kushiriki katika utafiti wa afya na kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Waandaaji walisisitiza dhamira yao ya kusaidia biashara mbalimbali, kuwapa wachuuzi wadogo wa ndani nafasi kuu katika tamasha hilo ili kuhakikisha kuwa wanaonekana zaidi.
3490007