IQNA

Kituo cha Kiislamu Austria chaanzisha mpango wa kuhifadhi Qur'ani kupitia intaneti

17:38 - May 15, 2022
Habari ID: 3475253
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Imam Ali AS cha Vienna, Austria kimeanzisha mpango wa kuhifadhi Qur'ani kwa njia ya intaneti.

Mpango huo uliopewa jina "Soma Qur'ani Nami" unahusu kuhifadhi Sura Yaseen katika Qur'ani Tukufu katika kipindi cha wiki 24.

Wanataka kushiriki katika mpango huo wanaweza kujiunga na Kanali ya Telegram ya kituo hicho ifuatayo:  https://t.me/izwien.

Washiriki wanasikiliza aya za sura hiyo zikisomwa na qarii maarufu wa Iran Hossein Esfehanian na kisha wanazihifadhi.

Sura Yaseen ni ya 36 katika Qur'ani Tukufu na ina aya 83 na maneneo 807.

Kituo cha Kiiislamu cha Imam Ali AS mjini Vienna, Austria kilianzishwa mwaka 1992 na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kustawisha Uislamu nchini Austria na pia kuwasilisha taswira ya Uislamu halisi kwa wasiokuwa Waislamu katika nchi hiyo.

4057136

Kishikizo: waislamu ، qurani tukufu ، imam ali ، vienna ، yaseen
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :