IQNA

Wasomi wajadili Nahj al-Balagha katika kongamano la Karbala

19:06 - May 03, 2025
Habari ID: 3480630
IQNA – Kongamano la wasomi kuhusu hadithi za Nahj al-Balagha ilifanyika katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq. Idara ya Uhuishaji wa Urithi na Dar-ul-Ulum ya Nahj al-Balagha, inayohusiana na Idara ya Mfawidhi wa  kaburi takatifu la HadhratAbbas (AS), iliandaa tukio hilo.

Kwa mujibu wa Lawa al-Atiyah, mkuu wa Dar-ul-Ulum, wasomi walioshiriki walijadili moja ya hadithi muhimu zaidi za Nahj al-Balagha, akiongeza kuwa madhumuni ya kongamano ilikuwa kuchunguza mitindo ya Isnad (kitendo cha kuunganisha mnyororo wa waliosimulia Hadithi) katika Nahj al-Balagha.
Aliongeza kuwa lengo lilikuwa pia ni kufufua urithi wa Imam Ali (AS) na kuonyesha maandiko ya Nahj al-Balagha katika jamii za Kiislamu kutokana na ushawishi wake mkubwa kwa karne nyingi.

Katika kongamano hili, msomi wa chuo cha Kiislamu au Hauzah Sheikh Arkan Al-Menahwi alielezea utafiti wake, ambao ulijadili usahihi wa hadithi hizo.
Alishukuru idara hiyo kwa kuzingatia urithi wa Kiislamu na kukuza utafiti kuhusu vitabu vikubwa vya Kiislamu, ikiwemo Nahj al-Balagha, Sahifah Sajjadiyah, na Risalat al-Huquq ya Imam Sajjad (AS).

Nahj al-Balagha ni mkusanyiko wa mihadhara, amri, dua, barua na semi za Imam Ali (AS) zilizoandikwa na al-Sayyid al-Sharif al-Radi takriban miaka elfu moja iliyopita.

3492909

captcha