IQNA

Vikao vya kusoma Qur'ani katika Haram ya Imam Ali (AS) huko Najaf

16:41 - January 13, 2025
Habari ID: 3480045
IQNA – Katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Imam Ali (AS), mjumuiko wa Qur'ani umefanyika katika Haram au kaburi takatifu la Imam Ali (AS) huko Najaf, Iraq kwa hisani ya kituo cha  Dar al-Quran katika eneo hilo takatifu.

Alaa Mohsen, mkuu wa taasisi hiyo ya  Dar al-Quran ametoa maelezo kuhusu hafla hiyo, akisema, “Mkutano huu ulihusisha usomaji wa Qur'ani Tukufu uliofanywa na wasomi maarufu, wakiwemo Abdullah al-Sailawi, Hassan al-Dhibhawi, na Karar Amama.”

Hafla hiyo ilivutia idadi kubwa ya waumini na ilijumuisha kupeana zawadi  kwa waliohudhuria.

Akisisitiza umuhimu wa mikutano ya Qur'ani, Alaa Mohsen ameongezea, “Matukio kama haya huchochea ukuaji wa kiroho kwa waumini, hasa ndani ya nafasi takatifu ya hekalu la Imam Ali (AS), linalojulikana kama 'Quran Hai'.

Dar al-Quran ya Haram ya Imam Ali (AS) mara kwa mara huandaa programu za Qur'ani, ikiwa ni pamoja na vipindi vya usomaji kila Ijumaa. Pia hufanya vipindi endelevu vya Khatm Qur'ani ili kukuza uhusiano wa kina na Qur'ani kwa waumini.

3491425

Habari zinazohusiana
captcha